Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s.) –ABNA– Mkuu wa Mamlaka ya Mahakama ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Hojjat al-Islam Gholam-Hossein Mohseni Ejei, amesisitiza umuhimu wa kulinda, kuimarisha na kudumisha umoja wa kitaifa na mshikamano wa wananchi.
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (IRNA), Ejei ameyasema hayo Jumatatu wakati wa kikao cha Baraza Kuu la Mahakama, kilichohudhuriwa pia na Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Amesema viongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu wamekuwa wakisisitiza mara kwa mara kwa kipindi cha miaka 47 umuhimu wa kulinda na kuimarisha umoja wa kitaifa na mshikamano wa wananchi.
Mkuu huyo wa Mamlaka ya Mahakama amewataka viongozi na wananchi kuwa waangalifu zaidi kuliko hapo awali ili kuhakikisha kuwa umoja wa kitaifa na mshikamano wa wananchi hauathiriwi.
Aidha, amesisitiza kuwa hakuna mtu anayepaswa kuruhusiwa kupenya katika safu za wananchi wenye nguvu na kusababisha fitina, migawanyiko na mifarakano.
Ejei pia amewataka wananchi kuwa makini zaidi dhidi ya wachochezi wa fitina, waenezaji wa uvumi na wanafiki, akisisitiza kuwa umoja na mshikamano wa taifa ni nguzo muhimu katika kukabiliana na changamoto na maadui.
Aliongeza kuwa katika suala la kulipiza kisasi dhidi ya adui, hakuna tofauti wala mgawanyiko miongoni mwa wananchi na viongozi wa Iran, bali wote wanapaswa kusimama pamoja kwa umoja na mshikamano.
Maoni yako